SERIKALI  imesema inatarajia kuanza kuyatoza kodi makampuni ya Google, Facebook, Instagram, Twitter, Apple na yote yanayoendesha huduma za mitandao ya kijamii nchini.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amendika wanafikiria kuanza kuwatoza kodi wamiliki wa makampuni hayo ya kigeni kwa sababu yanapata fedha na hayalipi kodi. Hata hivyo, Mwigulu amefafanua kuwa kodi hiyo haiwahusu watumiaji bali wamiliki wa makampuni hayo.

"Tunategemea (tunatafuta namna) kuwatoza kodi kama nchi zingine zinavyofanya kwa wamiliki wa Google, Twitter, Facebook, Instagram, Apple na Makampuni mengine kwasababu haya ni Makampuni ya Kimataifa na yanapata fedha kwa Watu wetu na hayalipi kodi. Kodi za Mitandao hazihusishi watumiaji (wananchi wanaotumia mitandao hiyo), hivyo watu wasipotoshe" Mwigulu Nchemba