MAmlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)imesitisha matumizi ya bei mpya za mafuta ambazo zimeanza kutumika septemba mosi 2021 na kuunda timu maalumu kuchunguza sababu za kupanda bei kwa kasi

Kaimu mkurugenzi mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kila jumatano ya kwanza ya mwezi bei mpya za mafuta hutangazwa

"Tumeamua kusitisha ili bei zilizopita ziendelee kutumika ambapoSerikali imeunda timu maalumu ya kuchunguza ,kuangalia kwanini bei zinaendelea kupanda,kwahiyo baada ya serikali kukamilisha kazi tutarudi tena kuja kutoa maelekezo mengine maalum" - Chibulunje.

TAARIFA KAMILI