Kassim Joseph mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa kijiji cha Namayakata mkoani Mtwara anashikiliwa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya kumshambulia Muksini Namkwacha kwa Panga na kupelekea umauti chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi baada ya Marehemu Muksini kulazimisha kupewa penzi na Dada yake Kassim au lasivyo apewe pesa zote alizompa.
Inaelezwa August 26 saa moja usiku Marehemu Muksini alikuwa na dada mmoja ambaye inasemekana kuwa ni Mpenzi wake na wakiwa kwenye mazungumzo walipishana lugha baada ya Muksini kumdai pesa zote alizowahi kumpa Mwanamke huyo kwa madai kwamba hataki kumpa penzi na ndipo kaka wa Mwanamke huyo aitwae Kassim Joseph alipoingilia kati na kumkata panga Muksin na kupelekea umauti wake .
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Mark Njera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Marehemu alikuwa amelewa na kulazimisha aondoke na Mwanamke huyo au arudishiwe pesa zake.
Kamanda Njera amesema Mwanamke aliyesababisha kifo amekimbia huku akiwataka Wananchi kuacha kujichukulia Sheria mkononi.
0 Comments