Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Urlich Matei amesema watuhumiwa hao walikamatwa mnamo septemba 5,2021 majira ya saa mbili usiku katika kijiji cha mabango, wilaya ya mbarali wakiwa kwenye harakati za kuwasafirisha watoto hao
Watuhumiwa hao ni Daniel Julius umri miaka 21 na Kamungu Julius umri miaka 30 wote wakazi wa wilaya ya Mbarali na kwamba wanadaiwa kuwachukua watoto 11 wanaoishi katika mazingira magumu na wengine kutoka kwa wazazi wao na kisha kwenda kuwauza .
RPC Matei amesema baada ya kuwafanyia mahojiano watuhumiwa hao walikiri kuwa walikuwa wakiuza kila mtoto mmoja kwa gharama ya sh.25 elfu hadi elfu 30.
0 Comments