Watu  watano wamefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la King'ori mkoani Arusha baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo waliofariki katika ajali hiyo ni abiria wawili na dereva mmoja ambao walikuwemo kwenye Canter na huku dereva na  kondakta ambao walikuwa kwenye Fuso.