Takribani wagonjwa 17 wamefariki baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko katika hospitali ya mji wa Tula huko Mexico
Baadhi ya wahanga walikuwa hospitalini hapo wakipatiwa matibabu ya uviko 19 kwa kutumia mashine ya Oxygen ,kabla ya kingo kupasuka ,maji kusambaa na kusababisha umeme kukatika
Wagonjwa arobaini 40 wamefanikiwa kuhamishwa na kikosi cha uokoajiwakati boti ikiyokuwa ikimsafirisha Gavana wa jimbo hilo Omar Fayad ilizama ingawa hakupata madhara na hali yake ni salama kama alivyoweka kupitia mtandao wa twitter huku akisisitiza kwamba mamlaka za serikssli zitaendelea kuratibu shughuli za dharura na uokoaji katika maeneo yaliyoathirika.
Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez Obrador amesema amesikitishwa sana na vifo vilivyotokea hospitali hapo hivyo Amewataka wakazi wa maeneo yaliyoathitika kuhama makazi hayo au kukaa na jamaa na marafiki katika maeneo salama
Zaidi ya watu30,000 katika miji mbalimbali nchini humo wameathiriwa na mafuriko hayo.
0 Comments