Takribani watu 41 wamefariki dunia nchini indonesia baada ya kutokea kwa ajali ya moto katika gereza la tangerang katika mji mkuu wa nchi hiyo ,Jakarta .

Moto huo umezuka asubuhi ya leo septemba 8 wakati wafungwa wengi wakiwa bado wamelala .


 KATIKA upande wa Block C ambako ndipo moto ulipozuka kulikuwa na jumla ya wafungwa 122  waliokuwa wakikabiliwa na kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

Kupitia taarifa iliyotolewa wafungwa wengi ni majeruhi huku baadhi yao wakiwa katika chumba cha mahututi (ICU).

Hadi sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana taarifa iliyotolewa na msemaji wa magereza wa indonesia inasema wanaendelea kufanyia uchunguzi suala hilo na ripoti kamili itatolewa baada ya uchunguzi huo.