Mchungaji mmoja huko nchini Nigeria aliyefahamika kwa jina la Cyril Utomi amechoma moto mawigi na vipodozi vya muumini wake wa kike kwa madai kuwa asingeweza kukutana na Yesu akiwa na nywele na vitu vingine vya bandia ikiwa ni pamoja na viatu virefu.
Utomi alichoma vitu hivyo katika mkutano wa mahubiri ulioandaliwa na Holiness Revival Movement Worldwide mwishoni mwa mwezi Agosti ambapo baada ya kuchoma vitu hivyo alichapishapicha zinazoonyesha hivyo vikiteketea kwa moto katika mtandao wa Facebook.
0 Comments