Kuelekea mchezo wa watani wa jadi wa ngao ya jamii utakaochezwa hapo kesho septemba 25 kunako dimba la Mkapa jijini Dar es salaam, shabiki wa klabu ya Simba Mc Mishepu anayeishi maeneo ya Kijitonyama jiji Dar ameamua kuweka bondi nyumba yake yenye thamani ya sh. milioni 300 endapo Simba itafungwa na Yanga kwenye mchezo huo.

Mc Mishepu amesema ameamua kufanya hivyo kwani anaamini Yanga hawezi kuifunga Simba hivyo ikitokea Simba ikafungwa afuatwe na atatoa hati za nyumba na kuwakabidhi mashabiki wa Yanga.