Mkuu wa mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakhar Kunenge ameagiza kurudiwa kwa tathmini ya malipo kwa fidia ya nyumba 15 za waliokubali kupisha upanuzi wa eneo la soko jipya la Chalinze mkoani Pwani.
Mheshimiwa Kunenge ameagiza hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Bwilingu Chalinze mkoani Pwani wakati akiwa kwenye ziara ya kazi kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Bagamoyo.
Kunenge amesema tathmini hiyo irudiwe kwa kuboreshwa sawa na hali halisi ya gharama za maisha kwa sasa maana hataki kusikia watu waliopisha maendeleo wakapate shida baada ya kukubali kujitolea.
0 Comments