Timu
ya Wanawake ya Simba, Simba Queens safari yake imehitimishwa hii leo baada
ya kupokea kipigo cha 2-1 dhidi ya Vihiga Queens katika mchezo wa nusu
fainali.
Kipigo
hicho walichokipata Simba Queens kinahitimisha safari yao katika
Mashindano ya CAF Women’s Champions League CECAFA Qualifiers kwa
mwaka huu 2021.
Mchezo
huo ulipigwa katika dimba la Nyayo stadium na kuwaacha Simba Queens
wakishuhudia Vihiga Queens wakitinga hatua ya fainali ya michuano
hiyo.
0 Comments