Majeshi ya Israel leo yameanzisha msako mkubwa kaskazini mwa nchi hiyo na katika Ukingo wa Magharibi baada ya wafungwa sita wa Palestina kutoroka usiku wa kuamkia leo kutoka kwenye gereza lililo na ulinzi mkali, katika tukio la nadra sana la aina hiyo.
Maafisa wanasema wameweka vizuizi vya barabarani na wanapiga doria katika eneo hilo.
Redio ya jeshi la Israel imesema wafungwa hao wametoroka kupitia handaki katika gereza la Gilboa.
Aidha Redio hiyo imetangaza wafungwa 400 wanaondolewa kutoka gereza hilo kama hatua ya tahadhari tu ili kuzuia jaribio la wengine zaidi kutoroka.
Naftali Bennett Waziri Mkuu wa Israel amelitaja tukio hilo kama la kijasiri na lenye kuhitaji juhudi kutoka idara zingine za ulinzi za Israel.
Wafungwa hao waliotoroka wanaaminika kwamba wanaelekea eneo la Jenin ambako mamlaka ya Palestina haina nguvu.
0 Comments