Waziri wa mazingira  Dr Congo anasema  karibu watu 4,500 wameugua kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia kuvuja kwa sumu kutoka kwa mgodi wa almasi katika nchi jirani ya Angola, .

Eve Bazaiba amesema watu 12 walikuwa wamefariki dunia na  kuwa DR Congo itauliza fidia ya uharibifu uliosababishwa lakini haikutaja kiasi.

 

Hata hivyo, hadi kufikia hivi sasa hakuna aliyesema chochote kujibu hayo hasa kutoka kwa kampuni ya madini.

 

Mwezi uliopita kulikuwa na uvujaji wa sumu kutoka eneo la uhifadhi wa bidhaa za vyuma vizito uliosababisha mto kuwa na rangi nyekundu, samaki, viboko na wanyama wengine wakafa.