MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Omary ambaye ni fundi wa kutengeneza samani (fenicha) amekutwa amefariki katika mazingira ya kutatanisha huku mwili wake ukiwa na majeraha kichwani na usoni pia ukivuja damu.
Mwili wa marehemu umekutwa katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam ukiwa umetupwa huku pembeni yake kukiwa na bisibisi pamoja na kalamu hali ambayo imewafanya mashuhuda wa tukio hilo kuhisi kuwa huenda ameuawa na watu wasiojulikana kwa kumshambulia na vitu vyenye ncha kali.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na Omary wamesema kijana huyo alikuwa mpole, asiye na makuu na mtu na wala hawajawahi kusikika kama ana ugomvi na mtu.
Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kuchukua mwili huo kwenda kuuhifadhi na kufanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo la kinyama.
0 Comments