Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amekabidhi misaada mbalimbali kwa waathirika wa tukio la moto lililoteketeza nyumba 20 za wananchi na mali zao katika kitongoji cha Shaurimoyo, kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwara Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Amekabidhi misaada hiyo wakati alipofika kijijini hapo kuwapa mkono wa pole kutoka halmashauri ya wilaya ya Rufiji na kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ambaye yupo bungeni kwa sasa.

Misaada aliyokabidhi ni pamoja na vifaa vya shule kwa wanafunzi 24 ambapo wanafunzi 22 ni wa shule ya msingi Shaurimoyo na wanafunzi 2 ni wa Shule ya sekondari ya Chumbi ambao wamepewa sare za shule, madaftari kulingana na idadi ya masomo yao, kalamu na peni