Muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen umesema watu wanane wamejeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani iliyolenga uwanja wa ndege wa Abha nchini Saudi Arabia.
Katika taarifa yao, muungano huo umesema kuwa waliojeruhiwa ni pamoja na raia mmoja wa Saudia, Mnepali, watu watatu kutoka India na watatu kutoka Bangladesh - mmoja wao akiwa katika hali mbaya.
Kundi la Huthi halikutoa tamko lolote hadi sasa kuhusu shambulio hilo.
Marekani imelaani shambulio hilo na kulitaka kundi la Huthi kukubali kukutana kwa mazungumzo chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.
Pande hizo mbili zimekuwa zikipigana tangu muungano wa kijeshi wa Saudi Arabia ulipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen 2015 kwa kuunga mkono upande wa serikali.

0 Comments