Antonio Nugaz (Mzee wa  Wape Salamu) amemaliza mkataba wake na uongozi wa Yanga umeamua kutomuongezea tena mkataba kuendelea na majukumu yake ya Ofisa muhamasishaji.

Taarifa hiyo imetolewa na klabu ya Yanga kupitia mitandao yake ya kijamii leo Septemba 1, 2021.

Kwa upande wake Nugaz pia ameushukuru Uongozi wa Yanga katika kipindi chote alichofanya nao kazi.

Tukio hilo la Nugaz limekuja siku chache tangu Klabu hiyo ipate Msemaji mpya aliyetokea Klabu ya Simba SC, Haji Sunday Manara.

Aidha siku tatu ama nne zilizopita, Nugaz katika mtandao wake wa Instagram alipost "video clip" inayomuonesha akifurahi na mashabiki wa Yanga huku akimuita jina ambalo sio Sahihi msemaji mpya wa Yanga, tukio ambalo linasemekana kuwakera Viongozi wa juu wa Klabu ya Yanga.