WALIMU WACHARAZWA VIBOKO NA WAFUGAJI KILOSA



Walimu watatu wa shule ya Msingi Malolo A iliyopo tarafa ya Mikumi wameshambuliwa na Wafugaji kwa kucharazwa fimbo chanzo kikitajwa Kuwa ni migogoro ya wakulima na Wafugaji .

Akizungumza na wananchi Katika mwendelezo wake wa kusikiliza kero za wananchi mkuu wa wilaya hiyo ya Kilosa  ALHAJ MAJD MWANGA Amesema tukio Hilo limetokea Katika kijiji hicho ambapo Wafugaji hao wanadaiwa  kuchukua mifugo kwa nguvu iliyokua imehifadhiwa Katika eneo la shule baada ya kulisha mazao ya wakulima ndipo wakatumia nguvu kuwacharaza VIBOKO walimu Ili kupora mifugo hiyo

DC Mwanga Amesema baada ya tukio Hilo polisi walifika Katika eneo Hilo kwa lengo la kuwakamata waharifu ndipo afisa mtendaji wa kijiji hicho Cha Malolo A bwana Baraka Noya akawataarifu Wafugaji wakimbie Jambo ambalo Jeshi la polisi likalazimika kumkamata na kumshikilia Katika kituo Cha polisi cha Mikumi.

KWA HABARI ZAIDI TAZAMA VIDEO HII



Post a Comment

0 Comments