Watu wanne wamefariki Dunia kufuatia ajali ya gari iliyohusisha Gari ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya kilwa Mkoani Lindi aina Toyota Nisan yenye namba za usajili T 503 APU na Basi dogo la Abiria aina ya Hiace lenye namba ya Usajili T 215DKA
Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya kamanda wa polisi wa Mkoa huo ACP Mtatiro Kitinkwi baada ya kuthibitisha kutokea tukio hilo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa bado hakijafahamika
Gari ndogo aina ya hiace ilikuwa inatoka Kilwa masoko kwenda Nangurukuru huku gari ya Mkurugenzi wa Kilwa ikiwa inatoka Nangurukuru ikielekea Kilwa masoko


0 Comments