Basi lenye namba za usajili T 703 DLG  Kampuni ya Emigrace linalofanya safari zake kati ya Babati na Dar es Salaam, limepata ajali leo asubuhi katika mlima wa Kolo, Kata ya Kolo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma
Kwa mujibu wa Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu saba wamepoteza maisha papo hapo ambapo kati yao ni wanaume watu wazima wawili na mtoto mmoja wa kiume, wanawake wawili na watoto wawili wa kike na majeruhi zaidi ya 30.
Miili ya watu hao imepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Kondoa huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa katika hospitali hiyo na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Mrara, Halmashauri ya Mji wa Babati.