MKUU wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)Dkt Frederick Shoo amesema ameona kazi kubwa zinazofanywa na kanisa hilo dayosisi ya maandalio ya Mafinga na kuwataka kuendelea na kazi ya Mungu wasirudi nyuma .
Dkt Shoo ametoa Kauli hiyo leo wakati wa ibada maalum ya changizo la ujenzi wa kanisa la Usharika wa Kinyanambo Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
Amesema kazi inayofanywa kwenye kanisa hilo ni kubwa na inaonekana na kuwa wasikubali kurudi nyuma wala kukatishwa tamaa na mtu katika kuifanya kazi hiyo ya Mungu .
Dkt Shoo amesema jitihada zinazofanywa kwenye kanisa hilo dayosisi ya maandalio ni kubwa na kuwa ameambiwa kuwa eneo hilo linajengwa kanisa la Ghorofa na kuna jingine limekamilika tena la Ghorofa.
"Niseme tu kazi inayofanywa ni kubwa sana katika eneo hilo na inaonekana pia nikupongeze sana askofu mstaafu wa KKKT dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegella kweli unafanya kazi kubwa sana kusimamia dayosisi hii ya maandalio kweli wahenga walisema nyani Mzee amekwepa mishale mingi nakupongeza " Dkt shoo
Amesema kuna thawabu kubwa kumtumikia Mungu japo wapo watu wanaamini kuwa wapo kwa ajili ya kumtumikia Mungu kwa faida .
"Futeni hayo mafundisho yanasema tumika ili ubariki bali toa kwa sababu na toa kwa kuwa "
Amesema wale wanaoingia kwa Nguvu zao badala ya kuponya wamekuwa wakizalisha machungu kwenye nafasi zao .
0 Comments