Na Hamida Ramadhan,Dodoma
KAIMU Mkurugenzi wa Magonjwa yasiokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Njinsia wazee na watoto Dkt.Shedrack Makubi amesema Takwimu zinaonyesha Tanzania kuna wagonjwa wa afya ya akili Milion 7.
Akiongea leo na waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya afya ya akili Duniani na siku ya kupinga matumizi ya unywaji pombe uliopitiliza Dkt Makubi amesema magonjwa ya akili ni mzigo mkubwa katika Taifa ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa katika jangwa la Sahara asilimia 13 wanaugonjwa wa afya ya akili.
"Tuko katika sehemu mbaya kama Takwimu zinavyoonyesha Milioni 7 ya watanzania wanaugua ugonjwa wa afya ya akili wakati Tanzania tuko milioni 60 ni ukweli usiopingika tuko sehemu mbaya," amesema Dkt Makubi.
Naye Mkurugenzi wa Hospitali yaTaifa ya Magonjwa ya akili Mirembe Inocent Mwombeki akiongea kwa niaba ya Waziri wa Afya Dkt Doroth Gwajima kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa upatikanaji wa huduma za magonjwa ya akili nchini bado sio wakuridhisha Kutokana na kuwepo kwa hospitali Moja tu nchi nzima ambayo ni hospitali ya kitaifa ya mirembe iliyopo jijini Dodoma.
"Utoaji wa huduma hizi inaonekana kuwa hafifu Kutokana na Watu kusafiri kutoka maeneo mbalimbali nchini kufuata huduma jijini Dodoma huku uwezo wa huspitali hiyo ukiwa na vitanda vya wagonjwa 590 pekeee," amesema Dkt Mwombeki
Aidha ameeleza changamoto nyingine zinazoikabili hospitali hiyo nipamoja na uchakavu wa miundombinu hasa ya majengo kutokanana hospitali hiyo kuwa ya muda mrefu huku akiitaja changamoto nyingine nipamoja na kuwarejesha wale waliopata nafuu kwenye jamii
Naye Mary Katanga mwakilishi kutoka Compation ametoa wito kwa serikali izidi kiboresha mifumo ya afya ya akili kwani kila kitu kinaanzia katika afya ya akili .
Amesema uelewa juu ugonjwa wa afya ya akili bado ni mdogo hasa kwa wao wanao wahudumia jamii ya watu wa chini.
0 Comments