KAMPENI YA "NIACHE NISOME" KUZINDULIWA OCTOBA 23 MKOANI MANYARA

Katibu Mkuu mtendaji wa Shirika La Elimika Simanjiro Lowassa Lomujey akiwa pamoja na Bi. Yamat ,muhamasishaji wa KAMPENI ya NIACHE NISOME.


 Na Rehema Abraham , Kilimanjaro

SHIRIKA lisilokuwa la Kiserikali la Elimisha Simanjiro, lenye Makao yake Makuu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, linatarajia kuzindua shirika Hilo pamoja na Kampeni ya 'NIACHE NISOME' ili Kupambana na ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuachishwa shule pindi wakiwa Bado hawajahitimu na kulazimishwa kuolewa.

Katibu Mkuu mtendaji wa Shirika hilo Lowassa Lomujey, aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itafanyika Oktoba 23 mwaka huu katika mji mdogo wa Simanjiro mkoani humo.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike katika kuhakikisha wanawaweka wawe katika mazingira wezeshi ya kusoma pasipo na changamoto wala vikwazo vyovyote.

Kwa upande wake muahamasishaji wa kampeni hiyo Elizabeth Yamat, amesema watoto wa kike wa jamii ya wafugaji wapo katika hatari zaidi, hali ambayo inasababisha wasipate elimu sawa kama wanavyopata watoto wa kiume.

"Tunajitahidi kwenda huko maeneo ya vijijini ambapo ndio Kuna wazazi ambao hawaeliwi umuhimu wa watoto wao kusoma,japo Kuna watoto wengine wanakataa kwenda shule lakini wanapoona Kuna msichana wa jamii hiyo labda ana elimu ya juu na yeye anahamasika kusoma ,Alisema Yamat."

Amesema watoto wa kike wa jamii ya wafugaji hawapewi kipaumbele cha wao kwenda shule, hivyo kampeni ya 'NIACHE NISOME' ni sauti ambayo itawafanya mabinti hao watamani kusoma ili waweze kusimama na kufanikisha ndoto zao.

Amesema kuwa kumekuwepo na taarifa nyingi za unyanyasaji kwa watoto na kwa kiwango kikubwa mwathirika mkubwa amekuwa ni mtoto wa kike hivyo zinahitajika juhudi za pamoja ili kumkwamua na kumuondoa katika hatari ya kukosa haki ya kupata elimu bora na kufikia ndoto zake.

Naye afisa ufundi na mahusiano wa shirika hilo Lucas Mandela, amewaomba wadau na wananchi kuendelea kuwaunga mkono katika kampeni hiyo ya kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu bora kwakuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha familia na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments