KILA MTU ANA MAUMIVU



EWE DADA

Natamani ningekufahamu na kukupenda kabla Moyo wako hauja jeruhiwa na wale walaghai wa mapenzi.

Natamani ningekuwa Mwanaume wako wa kwanza na wa mwisho niweze ishi na wewe kwa furaha na Nikuheshimu na kukupenda vile ulivyo.

Natamani ningekuwa na uwezo wa kufuta kumbukumbu zako za nyuma zinazokuumiza na kukutuliza kisha uweze kukumbuka nyakati tutakazokuwa pamoja.

Bahati mbaya nimekufahamu wakati Moyo wako ushaumizwa vya kutosha ,Umedanganywa mara nyingi na wengi ,Ushakata tamaa ya kupenda kila anaeongelea mapenzi unamuona Muongo.

Natamani ningekufanya uamini hisia zangu kwako kuwa ni za dhati Lakini maumivu uliyo nayo moyoni yanakufanya usinielewe..

Natamani ningekuwa na uwezo wa kukufanya uniamini na unipokee katika moyo wako na utambue kuwa nimefunzwa KUPENDA naogopa KUTENDA na Sito uchezea moyo na mda wako,Bali Nitavitunza

Naomba tambua

Nami NINA MAUMIVU kama yako
Ulitendwa na wanaume wenzangu
Nami nilitendwa na wanawake wenzako sote tuna maumivu hivyo tukiheshimiana na kuaminiana twaweza farijiana na kufikia ndoto zetu. Bado tunayo nafasi,karibu katika ufalme wa mapenzi yangu nikiwa Mfalme nawe uwe Malkia.

EWE KAKA
Natamani ningepata nafasi nikuoneshe kuwa wanawake hatupo sawa,tupo wenye mapenzi ya dhati ila hatuna bahati na Sifa zetu zinachafuliwa na wanawake wapenda pesa

Mimi mwanamke mtafutaji,kamwe sibweteki,nahitaji upendo na heshima wala sio vya mtu maana vyangu vinanitosha

KAKA na DADA

Sio peke yako unae umia
Wapo wengi huenda maumivu yao ni zaidi yako hivyo usiogope kuwapa nafasi kwa kigezo cha kuogopa kuumizwa.

Post a Comment

0 Comments