WANAWAKE LINDI WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO DUNIANI


Wanawake Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wameadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani kwa kufanya tafiti na kuiomba serikali kusimamia haki za mtoto wa kike kusisitiza kushirikishwa kwa mtoto wa kike katika dunia ya kidigitali huku haki zake zikiendelea kulindwa ikiwemo haki ya kupatiwa fursa ya elimu kwa uwiano ulio sawa katika Jamii Hususan Vijijini

Katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Kike Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi pamoja na tafiti mbalimbali kufanyika ambapo changamoto nyingi zilibainika ikiwemo Mimba kwa wanafunzi na ukosefu wa elimu ya malezi bora ya watoto wa kike ambapo baadhi ya walezi ikiwemo walimu kuanza mahusiano kutokana na Vishawishi mbalimbali
Akizindua warsha ya uwasilishaji wa changamoto zilizo katika Jamii kufuatia Tafiti za Jukwaa la wanawake kilwa(TUJIWAKI)Katibu Tawala wa wilaya ya Kilwa Haji Mbaruk Balozi aliitaka jamii kubadilika na kusaidia serikali kumwendeleza mtoto wa kike kwa kuhakikisha vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto wa kike vinafikishwa katika vyombo vya usalama Ambapo kwa sasa serikali ina mikakati mbalimbali inayochukua kukabiliana na vitendo hivyo viovu
PILI KULIWA Katibu wa Jukwaa la wanawake wilaya ya Kilwa(TUJIWAKI)Pamoja na wadau wengine Akiwemo mratibu wa Dawati la Jinsia wilayani Humo WP Mariam Raymond
Wakiongea katika warsha hiyo wamebainisha kuwa katika utoaji wa elimu ya haki ya mtoto wa kike wamebaini kwamba shughuli mbalimbali za kijamii zimekuwa na urithi mbaya kwa watoto wa kike na kuwavurugia maisha yao ya baadae.

Katika Tafiti hizo jumla ya watoto wa kike 1760 walifikiwa 1200 wakiwa wa shule za Msingi na 560 sekondari ambapo kupitia miradi inayowezeshwa na Action Aid na TCRS Inasaidia kuwajengea uwezo watoto kujiengua na shida iliyopo katika jamii hasa afua za kuwawezesha kutimiza ndoto zao ambapo Kilwa inaongoza katika utelekezaji watoto kutokana na familia kutengana na kuleta adha kubwa kwa watoto ikiwamo kufanyiwa ukatili na kushindwa kuendelea kiasi cha wao kuingilia kati.

Post a Comment

0 Comments