Katika maisha yako Hakuna hali iliyo ya kudumu ,iwe furaha au huzuni bado kuna muda utafika mambo yatabadilika tu.
Usitumie mda wako mwingi kujilaumu au kulaumu kwa hali yoyote ile ,utawalaumu wangapi na utajilaumu Mara ngapi ,jambo la msingi ni kusonga mbele huku ukirekebisha makosa ya nyuma.
Tambua kuwa wapo waliowahi kupitia kipindi kigumu kuliko wewe lakini leo hii kila kitu kwao kipo sawa na maisha yanaendelea.
Wewe sio wa kwanza kuachwa/kuacha , kufeli,kuumizwa wala kudharauliwa.
Futa machozi,Simama ili uwaoneshe ubora wako ,Acha kuwa dhaifu na mnyonge badala yake Vaa nafsi yenye nia na ujasiri ili kukabiliana na changamoto zote.
Ukiamua unaweza tu siku zote Usiendeshwe na mtu mwenye lengo la kukuona ukianguka na yote kwa yote kwa imani yako usisahau kumshirikisha Mungu wako.
0 Comments