Ukimpata anae kupenda kukuheshimu kwenye mapenzi basi Kuna mda yatakufanya uone dunia yote mali yako kwa furaha utakayoipata,Utahisi Dunia nzima wewe ndiye unaye pendwa kwa dhati wengine wanaigiza tu ,Huwez pokea hata ushauri wa wengine maana utahisi ni wivu wao tu
Yatapo kuchachia
Utahisi dunia nzima umeibeba mgongoni kwako kwa simanzi na upweke utakaopata Utajikuta ukimchukia kila mtu ambae anajaribu kukushauri Utahisi huna thamani tena katika hii dunia, utakapowaona wengine wakifurahia mahusiano yao basi utazidi kuumia.
Hayo ndo Mapenzi Yakikunyookea furahia na shukuru Mungu Lakini yakikuendea ovyo basi piga magoti usali na kuomba simanzi iishe haraka sana.
Pamoja na hayo Wewe unayeonekana kupendwa sana leo basi usijisahau na kujiona huwezi achwa. Kuna walio pendwa na kujiona MALKIA/MFALME walipewa kila zawadi na kudekezwa kwa kila aina ila leo hawana tena hamu na mahusiano hayo Wanalia tu
Nawe uliyeumizwa Acha kujitesa juu ya mtu ambae ameamua kujitoa na kukuacha. Hakuzaliwa kwa ajili yako muache aende.
Usiwaze muda ulio poteza Sahau Posa na mali uliyo toa au kutolewa,kamwe usiumie juu ya pete mlizovishana au mlishazaa kwani mtabaki kuwa wazazi.
Hebu fikiria kesho yako pasipo yeye ,Utafurahi,Utakula.Utavaa bila msaada wake pia Kesho utapenda au kupendwa tena na kisha kuanzisha familia yako.
Jifunze kukubali kumuacha aende
0 Comments