Huenda una mume,mke au mpenzi Jitahidi uweze kumuheshimu na kumthamin wala usimuone wa kawaida hata kidogo kwani Hivyo alivyo wapo ambao wanatamani wangepata bahati ya kuwa nae waweze kumfanya bora kwa mengi.
KAKA umepata Mpenzi au mke ambae mzuri ana jishughulisha lakini pia ana jiheshimu. Lakini wewe unafanya uhuni mpaka hawara zako wanadiriki kumpigia simu za kumtukana. Akikuuliza unamjia juu hata kumpiga.
Kaka unajiona mzuri sana au una pesa kumpata mwanamke yoyote. Ila kumbuka kuna rafiki zako ambao wanatamani wangepata mke kama wako hakika wangefurahi.
Tulia KAKA na mkeo na kama unaona bado huwezi kutulia basi usimtese mtoto wa watu
DADA una jamaa ambae huenda hana mvuto lakini ni mtafutaji na ana kupenda kwa dhati. Lakini wewe eti huwezi ishi nae unatumia tu pesa zake.
Una mume ambae analala porini kutafuta pesa ili ule, uvae lakini wewe unatumia kama nafasi kuwapa penzi vijana wavaa milegezo na wanyoa viduku eti ndo wana mvuto.
Mumeo anakupa mtaji unaishia kula, kuvaa kisha unaishiwa
Kuna mdogo ,dada, ndugu yako ambae hapendi unavyo ishi na mumeo. Wanajua umepata mume bora ila we sio mke bora wanatamani Wangeipata hiyo nafasi basi wangefurahi na kutulia.
Kaka na dada.
Linda uhusiano wako Uliye nae siku ukimpoteza ndo utaelewa kiasi gan alikuwa muhimu kwako. Mbaya zaid atokee kwako afu aende kwa mtu wa karibu yako na wakaishi vizuri, hakika utaumia.
Muheshimu uliye nae Usijifanye huoni Upendo wake ,Uvumilivu wake ,Maumivu yake.
Kumbuka Anapendwa na wengi ,Anatakwa na wengi ,Anajiheshimu ndo maana bado yupo nawe,ila siku akiamua hakika hutomtuliza
Hivyo usichukulie poa
0 Comments