Shirikisho la soka Tanzania limetoa bei za viingilio katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia kati ya Taifa stars na Benin ambapo VIP B na C ni sh.5000 na kwa mzunguko ni sh.3000.

Pia limesema wameruhusiwa kuingiza mashabiki elfu 10 kushuhudia mtanange huo.