Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kesho itakuwa dimbani kukipiga na Benin kunako dimba la Benjamini Mkapa majira ya saa 10:00 jioni katika mechi ya kuwania kufuzu kwa fainali ya kombe la Dunia nchini Qatar 2022.
Kuelekea kwenye mchezo huo kocha wa Taifa stars Kim Paulsen amesema anawaheshimu wapinzani lakini ana imani ya kushinda.
"Tunawaheshimu timu pinzani ,lakini tunaamini tutashinda.. Tunataka kuongoza kundi kama ilivyo sasa".
Naye nahodha wa kikosi Stars John Bocco amesema wanajivunia kucheza kwenye ardhi ya nyumbani ambpo mara nyingi wanapata matokeo.
"Kikubwa tunachojivunia ni tunacheza katika ardhi ya nyumbani, na mara nyingi tukicheza nyumbani tunapata matokeo mazuri".
Stars wataingia katika mchezo wao huu wakiwa vinara wa kundi J kwa jumla ya alama 4 sawa na wapinzani wao Benin.
0 Comments