MWANAMKE MWEMA NI ZAWADI MSHIKILIE ASIKUPONYOKE


Kaka au baba Usimuache Mwanamke Ambaye Anayepigania Maendeleo Yako Tambua Dunia Haikuletei Mke Mwema Mara Mbili Akiondoka Tuu Huyo Basi Umekwisha

Tambua Yeye Ni Mlinzi Wako Kinyota Na Kimaombi Uwapo Kwenye Kutafuta Riziki Kama Vile Kazini, Biashara N.K 

Usiuumize Moyo Wa Mkeo Makusudi Na Ukimkwaza Basi Kimbia Haraka Umuombe Msamaha Kabla Hajakunja Moyo Wake Utaona Magumu Fulani Maishani Mwako Tambua Mwanamke Ni Kiumbe Dhaifu Aliyeletwa Na MUNGU Kutukamilisha Sisi Wanaume

Tambua Ule Udhaifu Wake Wa Mwanzo Huondoka Pindi Akutanapo Na Mwanaume Mwenye Kujua Wajibu Wake Kwa Mke Na Kuzingatia Maagizo Ya MUNGU Juu Ya Upendo Na Heshima Kwa Wanandoa

Tujifunze Kuwathamini, Kuwajali Na Kuwapa Heshima Wake Zetu ili Nao Watutii Katika Mambo Yote Ndipo Tutakapobarikiwa Na Kujaa Mafanikio Ya Kiroho Na Kimwili

Post a Comment

0 Comments