Rais wa Jamhuri ya Burundi Evariste Ndayishimiye, amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia leo tarehe 22 hadi 24 Oktoba, 2021.
Rais Ndayishimiye amewasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kuelekea Ikulu ya Chamwino ambako atakuwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino, Rais Ndayishimiye amekagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21 kwa heshima yake na baadae viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na kufuatiwa na mazungumzo rasmi.
0 Comments