SIO BUSARA KUJISIFIA UPUMBAVU


KENGE hukimbia manyunyu ya mvua au matone ya maji na kujitumbukiza ndani ya mto maana ndivyo akili yake inavyo mtuma akiamini kuwa maji ya mto ni bora kuliko mvua
 
Kuna wakati WANAUME huwa wana akili na mawazo yasiyo na maana japo wao huona ni sifa kwa wakati huo.

MWANAMKE wako amekuvumilia kwa mda wote wa kipindi kigumu na kuna wakati alijinyima ili akusaidie wewe ,alikubali kukopa ili akupe mtaji au atatue shida zako lakini leo umefanikiwa unamuona MKEO hafai tena,pesa ulizo pata kwa msaada.wake wa hali na mali leo wazitumia kwa anasa na WAREMBO ambao kipindi huna walikukana au hawakujitokeza .

Unamuacha MWANAMKE ambae ana kushauri namna ya kutafuta pesa una mfuata  MWANAMKE ambae.ana kushinikiza utumie pesa.

MWANAMKE hajawahi kuomba hata senti tano yako umemuona hafai ila leo unafilisiwa na MWANAMKE ambae hana malengo nawe ana taka hela zako tu

Mwingine tayari una.MKE ila una jifanya hukamatiki,familia yako ina teseka.huku wewe upo bize kuhudumia kwingine halafu pesa zitapokaisha unarudi mpole kwa mkeo. 

Kuna wakati Mkeo anatamani bora usipate mshahara maana kila ukipata ni kero kwa ulevi na kuchepuka

Eti unataka mwanamke mrembo,mwenye makalio makubwa ambayo mkeo hana,hivi
HIPS pana ndizo zitawafanya kuwa BABA NA MAMA BORA.??? Je,Uzuri wake ndio utakaoongeza kipato cha familia?

Sio busara kujisifia UPUMBAVU

MUNGU wasimamie  ambao hawajawahi kingia katika NDOA waweze kupata wenza watakaoweza kushirikiana nao kujenga uchumi na familia,hata wanaolia na NDOA zao waonyeshee milango ya kuondokana na maumivu.

Maisha ya NDOA hayana kanuni bali kumuomba MUNGU Kulingana na imani yako.

Uliye katika Ndoa ishi kwa tahadhari kama mambo kwako mazuri mshukuru Mungu,kama ni magumu muombe Mungu.

Post a Comment

0 Comments