Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumzia kuhusu utoaji wa Elimu juu ya Chanjo ya UVIKO 19 kwa Wananchi. |
Na,Amon Mtega ,Ruvuma.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Bregedia Jenerali Wilbert Ibuge amewataka Viongozi wa taasisi mbalimbali wa Mkoa huo kwenda kutoa elimu kwa Wananchi juu ya chanjo ya UVIKO 19 ili Wananchi hao waweze kuchanja kwa hiari .
Wito huo ameutoa wakati wa kikao cha dharura cha mpango jamii shirikishi na harakishi juu ya upataji wa chanjo hiyo kwa Wananchi ili kuwafikia wengi kwa haraka zaidi.
Ibuge akizungumza kwenye kikao hicho kilichojumuisha viongozi wa makundi mbalimbali wakiwemo wa dini katika mkoa huo amesema kuwa mpango huo tangu mpango huo shirikishi uanze umeweza kuleta mafanikio makubwa ambapo takribani Wananchi 6,763 wamechanja ikiwa ni sawa na asilimia 22 katika siku 49 .
Amesema kuwa kama elimu itatolewa kikamilifu juu ya chanjo hiyo basi Wananchi wengi watachanjwa kwa hiari kwa kuwa elimu watakuwa wamepatiwa .
Mkuu huyo amefafanua kuwa kwa mujibu wa watalaamu wa Afya wamesema kuwa chanjo hiyo itamsaidia mwananchi akipatiwa na ugonjwa wa Corona kutokuathirika zaidi tofauti na ambaye hajapatiwa chanjo hiyo.
“Ombi langu kwenu pamoja na wananchi kupitia mpango huu shirikishi na harakishi mpokee elimu hii ili kila mwananchi aweze kuwa na uelewa kwa kuwa kuokoa maisha ni vita”amesema mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Jairy Khanga amesema kuwa elimu inaendelea kutolewa kwa kuhamasishana kwenda kwenye makundi mbalimbali ya jamii jambo ambalo kwa sasa muitikio kwa wananchi umeanza kuwepo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Ruvuma Nuru Ngereja akiwapongeza Wataalam wa Afya ngazi ya mkoa kwa kukuzunguka kutoa elimu ya Chanjo ya UVIKO 19 kwa Wananchi. |
Wadau mbalimbali akiwemo mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga mji Grace Quintine wakifuatilia kwa umakini maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na Wataalam wa Afya kuhusu Chanjo ya UVIKO 19. |
Katibu Ngereja licha ya kutoa pongezi hizo amesema kuwa ofisi yake itahakikisha kila mikutano inayofanyika ya chama itakuwa inawashirikisha watalaamu wa Afya kwa kuwapatia nafasi ya kutoa elimu juu ya chanjo hiyo ya UVIKO 19.
0 Comments