Ujana Una mwisho wake hata Babu na Bibi WA Leo nao waliwahi kuwa vijana.

Mwanaume unatakiwa kuwa na busara na maamuzi sahihi kwa wakati sahihi na sio kulingia maumbile ya kiume ambayo umejaaliwa.

Kwa kukosa busara WANAUME wengi huwa wanaona ni ujanja kumtelekeza mwanamke na mimba anahangaika kulea yeye yupo bize na wengine ila Siku akijifungua anaanza kumtamani mtoto kisa ni mzuri kuliko watoto wake wote au anaanza kumlilia warudiane kisa kapendeza.

Usijidanganye kuwa utakuwa kijana milele uzee unakusubiri usiwaze tu ngono mda wote inabidi uelewe kesho unahitaji kuwa na familia.

Acha maisha ya kuigiza ya kuwa na watoto wengi wakati hata sabuni yako hawaijui Hata kama mwanamke huwezi kuishi nae basi saidia huduma za mtoto .

Tambua kuwa Mwanamke hata awe amezalishwa watoto 2 ili mradi anajitunza na kujiheshimu bado anaweza kuolewa tena na MTU bora kuliko hata wewe uliyemzalisha..

Hii huitwa umempiga chura teke kumfanya afike alipo pangiwa na Mungu.

Narudi kwako  dada uliyezalishwa ukaachwa hata usikate tamaa kama unajimudu kumtunza mtoto pambana usimlazimishe  jogoo kuangalia vifaranga vyake maana Asije pata kisingizio cha kutaka kukupora mtoto.

Kuoa na kuolewa kupo tu kama Mungu kapanga hakuna wa kupangua

Kujiremba na usela kuna ukomo wake tutafute maisha na wenza sahihi katika maisha wakati miili bado INA nguvu  achana na maisha ya kuigiza .

Tuishi tukijua kesho tutakosa nguvu