Kwenye Maisha ishi kwa ajili ya kesho yako,
Siku zote tambua kuna kifo na kuondoka kwako kunaweza acha pengo kwa wategemezi wako.

Mshahara wako usikupe kiburi  kwani haijalishi unalipwa pesa nyingi kiasi gani hata kama umesoma sana ila tambua wanao hawawezi kurithi Kazi unayofanya. 

Tambua kuwa pindi utakapofariki bosi wako atamtafuta mbadala wako hata kabla ya mazishi yako  na Kama ulikuwa unaishi ndani ya nyumba ya shirika au taasisi mapema sana familia yako itafukuzwa na kuingia mtu mwingine.

Katika ulimwengu huu elewa kuwa Urithi sahihi kwa watoto wako ni Biashara na Elimu pekee maana Ukiwa na biashara au miradi mingi ni rahisi kuja kuendelezwa na wanao. 

Watu wengi wenye mafanikio mpaka sasa wanaonekana matajiri wakubwa ni kwa sababu wameendeleza kilichoachwa na wazazi wao.

Elimu pia itamfaa mwanao kabla ya kumfundisha pesa basi mpe kwanza nafasi ya kujitambua huenda baadae akawa mzuri zaidi.

Tusiridhike na mishahara ya kila mwezi ambayo  huisha hata kabla ya kwenda benki.  

Kwa kidogo unachopata waweza kufikiria biashara hata kama kila siku utakusanya elfu 2 kama mauzo inatosha.

Ila yote kwa yote mshirikishe Mungu kwa kila jambo kwa imani yako naye atakuongoza kufika unapopatarajia.