Pesa au ZAWADI inaweza kufanya uwe na idadi kubwa ya wapenzi.
Wapo watakaokufuata wenyewe na wapo utakao wafuata lakini kumbuka wote wanaonesha kukupenda kwa kuwa una pesa ,elimu, biashara zako au una mvuto kwa maana Handsome MWENYE kimo na rangi ya kuvutia..ila ulio nao kati yao huenda hakuna unae mfikiria kudumu nae.
Dada huenda umebarikiwa makalio makubwa sura nzuri na rangi yenye mvuto ndio maana wanaume wengi Wanakufuata hivyo inakuwa sababu kila MTU anakuja na ofa nzuri unajikuta kila MTU unamkubalia na kufanya nae mapenzi.
Ifike kipindi vijana tujue malengo yetu ni kutengeneza familia anasa haziwezi kuisha jiulize ni wanaume wangapi walikuja kwako kwa nia ya kukuoa uliwadharau ila Leo hii wanafurahi na ndoa zao wakati wewe bado unapumuliwa na waume za watu?
Ni wanawake wangapi uliwahi kuwa nao watulivu kwa tabia na walikuwa tayari kuishi nawe kwa hali yoyote ila Uliwaacha ukawafuata wazuri au wasomi ambao wamekufilisi mpaka mawazo ya uliye muacha ambaye Leo kaolewa ,kazalishwa au kachumbiwa halafu ndipo unaanza kuumia.
Bado hujachelewa Mungu hutupatia funzo kwa njia nyingi bado unayo nafasi kubadilika na kuweza kupata MTU sahihi chamsingi Jiamini kuwa wakati wako utafika nawe kuoa au kuolewa.
VIJANA mioyo yetu ina majuto maana tulishawakosea na kuwapa huzuni watu waliohitaji Faraja na upendo wetu tujitahidi tuepuke kurudia makosa.
MWANAMKE anaejitambua anahitaji umpende kwa dhati na umuheshimu huku ukimpa nafasi ya Uhuru kwako ,ishi nae kama rafiki sio kama kuruta wa jeshi muda wote ubabe.
MWANAMKE mpumbavu huwa na mawazo finyu bila malengo ,wazazi wake hata baiskeli hawana ila yeye anataka mwanaume mwenye Gari hata kama mume wa mtu anachowaza ni ngono na starehe kuliko kutafuta pesa..
Umri unaenda tutulie tutapata wenza ,bado unayo nafasi kurudisha heshima yako na familia yako,unaweza kuwa baba bora au mama bora.jifunze kupitia uhusiano wako uliovunjika wakati kila MTU alijua mngeoana.
Usimchukie kisa Ameolewa au Ameoa,Amezalishwa au amezalisha Bali jilaumu wewe mwenyewe kwa kukosa MSIMAMO na kumuamini yeye tambua kuwa mpaka anafanya hayo ameumia sana .
Tusipende tu kutoa lawama nasi tukiri tulipokosea
0 Comments