Kwa kiasi kikubwa mahusiano  mengi na ndoa kwa sasa huyumba pale matarajia yanapo kuwa tofauti..

Mwanaume anaamini kuwa akioa mwanamke mwenye kazi basi watasaidiana kulea familia na majukumu kupungua ila inapotokea mke hatoi pesa yake hata kwa mahitaji madogo ugomvi huanza.

Mwanamke nae huamini kuwa akiolewa na mtu Mwenye pesa basi ataishi kwa raha.atakula na kuvaa vizuri basi ikitokea ikawa tofauti ugomvi huzuka.

Wapo walioolewa na wanaume  wenye kazi nzuri lakini mke anajikuta anauza mkaa wa kupima ili ale na kuvaa ,Wengine huuza genge hata walioolewa na wafanya biashara wakubwa wameishia kuwekwa madukani kusimamia tu bila Uhuru wa kutumia pesa, Wengine wamejikuta katika majaribu kuwatoa kafara ndugu zao ili biashara zikue

Wapo  wenye wake wenye kazi na mshahara lakini mume anajikuta yeye ndo anawajibika kwa kila kitu hata chumvi Mke mshahara wake huwa kuvaa na kwenda saluni.

Kaka na dada

Unapoamua kuoa au kuolewa na mtu usifikirie kuwa kazi yake itakunufaisha. Kutoa ni moyo wa mtu Anaweza kuwa na kingi ila akakubania au atakuwa na kidogo ila atakufanya ule vizuri na kupendeza.

Mkeo au mumeo mtarajiwa anaweza kuwa hajasoma,hana kazi nzuri lakini anajua biashara nyingi Ukimuwezesha huenda kesho akawa na pesa kuliko wewe uliyesoma sana, Nawe utakaewezeshwa basi jitahidI kesho usibadilike baada ya kupata pesa

UJUMBE

Pesa zinatafutwa na familia inajengwa na watu kila  mmoja ajitoe kulingana na uwezo wake.. 

Pia kumbuka kuolewa au kuoa isiwe sababu kuzuiana kusaidia ndugu na familia kama wazazi.

Mwenye pesa na kazi nzuri sio lazima awe mwema na mtoaji. Kuna mda mwenye kipato kidogo anaweza kuwa msaada kwako kuliko Mwenye  pesa nyingi.

Maisha kusaidiana kikubwa muheshimu na mthamini mwenye nia ya kukusaidia na kukuinua toka ulipo.