DADA au KAKA,

Huwa inatokea katika mahusiano Mwenzako kila anapogusia suala la Ndoa na kuishi pamoja wewe unaonekana kutokuwa tayari kwa huo mda.

MWANAUME atasema: bado sijajipanga kimaisha,ngoja kwanza nivumilie kdogo

MWANAMKE atasema: mi bado sijafikiria kuolewa kwa sasa labda miaka 2 ijayo.

Kila mtu hutoa sababu za hapa na pale ili mradi kutofanikisha lengo Baada ya hapo mahusiano yanaendelea miaka inaenda . 

Inatokea siku mmoja kumwambia mwenzake kuwa Amepata Mtu wa kuishi nae na wapo katika mipango ndipo Sasa wewe unaanza kumjia Juuu na kudai kuwa Amekusaliti alitakiwa akusubiri wewe.

Swali kwako Dada au kaka

Akusubiri mpaka Lini? 

Wangapi walikusubiri kisha ukaishia kuwapotezea tu mda?Mnaishi mkoa au wilaya moja kila wiki mwezi mnaonana kwa miaka 2 au zaidi bado hujamfahamu?

IPO hivi

Ukiona aliye kuwa mpenzi wako kafanikiwa Kuoa au Kolewa muache aendelee na familia yake na usihesabu kama amekusaliti. 

Ana sababu zake kutofunga ndoa nawewe ,hata kama utaumia ila muache na maisha yake.Sio lazima kuwa angekuoa au Uolewe nae, haikuwa ridhiki yako muache

Ushauri

Unapomfanya akusubiri kwa mda mrefu utakuta mawazo yake na malengo kaweka kwa mtu mwingine,

Kila mtu anatamani apate mtu wa kuishi nae na sio kupotezeana muda.

Lakini pia usikurupuke kuishi nae mtu,hakikisha ushajiandaa hata kwa mtaji wa genge ili maisha yaende mkiwa pamoja ,Usifikirie kuwa kuoa au kuolewa kutapunguza ukali wa maisha.

Tamaa ya kutaka kuoa au kuolewa isikufanye umpe nafasi mtu ambae bado humfahamu vizuri mienendo yake,yaan umemfaham miez 3 unaanza waza kuishi nae

Pia ni hatar sana kupanga mipango ya ndoa na watu 2 au zaidi ukidai unawalinganisha. Utajikuta ukiishia sehemu mbaya na kujuta. Kuwa na mmoja ndiye ujaribu kumtengeneza na kumuandaa

Tahadhari DADA

Kama umepata mwanaume ambae kaonesha nia ya dhati kukupenda na yupo tayari kujitambulisha,wala usisite kumpa nafasi .

.Usimuamini mtu aliye kufanya usubiri miaka 3 eti atakuoa . unaweza msikiliza ukaachana na Mwenye malengo nae halafu ndipo nae huyo atakapoanza kukusumbua baada ya kuku haribia

Panga mipango ya maisha na mtu mwenye nia ya dhati ya kupata mwenza.

Epuka  mtu ambae hana malengo nawe.