Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema baraza limezishauri mamlaka husika kuwachukulia hatua wote waliohusika na udanganyifu huo.
“ Baraza limezishauri mamlaka kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kutokea kwa udanganyifu katika mitihani” Dk Msonde.
Msonde amesema pia baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 128 ambao waliugua au kupata matatizo na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au baadhi ya masomo
Watahiniwa hao wamepewa fursa nyingine ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mujibu wa kifungu 32(1) cha kanuni za mitihani.
Kupata matokeo: BONYEZA HAPA KUANGALIA
0 Comments