Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linawashikilia watu wawili jamii ya wafugaji kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Mwenyekiti wa umoja wa wakulima wa mpunga Ruvu CHAURU Chacha Sadala.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini kibaha Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema Sadala ni mkulima mwenye umri wa miaka 48 ambapo watuhumiwa wanaoshikiliwa ni wakazi wa kijiji cha Kidogozelo Kata ya Vigwaza Wamasai na wafugaji Petro Ngilango (26) na Robarti Kambei (28).
Wankyo amesema kwamba tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka huu majira ya saa 9:30 alasiri katika mashamba yanayomilikiwa na chama cha Umwagiliaji Ruvu CHAURU watuhumiwa hao na wenzao watatu jumla wakiwa watano walilazimisha kuingiza mifugo yao kwenye mabwawa ya kilimo cha umwagiliaji Ruvu ili ng'ombe zao zinywe maji.
0 Comments