Na Amon Mtega, Mbinga.
MAMIA ya Wakazi wa Jimbo la Mbinga mjini Mkoani Ruvuma wamejitokeza kwenye fainali ya mpira wa miguu ya kombe la Mbunda (Mbunda Challenge Cup) yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Jonas Mbunda .
Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za kutoka kwenye kata 19 za Jimbo hilo yamefikia tamati kwa fainali ya kuikutanisha miamba miwili ya timu ambazo ni Lusonga Fc na Masumuni Fc ambapo Masumuni iliibuka kwa bao moja katika kipindi cha pili dk 78 kupitia mchezaji wake King'anya Ibra jezi namba 10 mgogoni.
Akizungumza mgeni rasmi kwenye fainali hiyo ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo amesema kuwa mashindano hayo yameleta changamoto kubwa katika Wilaya hiyo na kuwafanya wakazi wake kuchangamka.
Huyu ndiye Mchezaji King'anya Ibra wa timu ya Masumuni fc aliyeipatia ushindi timu yake katika dk 78.kwenye fainali ya Mbunda Cup. |
Mkuu akigawa zawadi kwa timu hizo timu ya kwanza iliyochukua ubingwa ni Masumuni Fc ambayo imechukua kitita cha sh.Laki sita(600,000) pamoja na kombe huku mshindi wa pili ambayo ni Lusonga Fc alijinyakulia Sh.Laki Nne (400,000).huku timu ya tatu imepata Sh.Laki tatu(300,000 )na yanne imepata Sh.Laki moja na elfu Hamsini (150,000)na zenyewe pia zilipatiwa zawadi pamoja na timu ambazo zilishiriki na kutolewa zilipatiwa zawadi za sh.Elfu Hamsini (50,000).
Mwenyekiti wa Chama Cha mpira Wilaya ya Mbinga ,Ahamad Mwalimu akizungumzia jinsi mashindano hayo yalivyoleta hamasa kwenye Wilaya hiyo. |
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha mpira Wilaya ya Mbinga (FAMBI) Ahamad Mwalimu awali amesema kuwa mashindano hayo yalianza Oktoba tatu mwaka huu na tamati Novemba 14 mwaka huu huku vituo vinne vilitumika ambavyo ni Kihungu,Kilimani,Beterehemu na Tanga.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa mashindano hayo yamefanyika kwa mfumo wa mzunguko na hatimaye kufikia kilele cheke kwenye fainali ambayo timu ya Masumuni Fc imeibuka mshindi dhidi ya Lusonga Fc.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Beda Hyera akizungumzia jinsi ilani ya CCM inavyotekelezwa kwa vitendo kupitia Mbunge wa Jimbo hilo Jonas Mbunda. |
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Beda Hyera amesema kuwa ofisi ya Mbunge imefanya jambo jema ambalo linatakiwa kuungwa mkono kwa kuwa linatekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM kwa vitendo.
Hata hivyo katibu wa mbunge wa Jimbo hilo Simoni Ponera (Doto)akizungumza kwa niaba ya Mbunge huyo amesema kuwa wanazipongeza ofisi zote za Serikali ikiwemo ya mkuu wa Wilaya na ya Mkurugenzi wa Mbinga mji Grace Quintine kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye ofisi ya Mbunge.
Simoni Ponera ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda akizishukuru taasisi za Serikali kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye ofisi ya Mbunge.
1 Comments
Hongera Sana mh Mbunda Mbunge wa Mbinga mjini , kwakuendeleza na kukuza vipaji kwa Vijana na kutengeneza fursa za ajira kwa Vijana.
ReplyDelete