OFISI YA ELIMU SEKONDARI MBINGA YAWEKA MJI YAWEKA MIKAKATI KUIBUA VIPAJI VYA MICHEZO KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI.


Afisaelimu Sekondari Halmashauri ya Mbinga mji Stuart Kuziwa akizungumzia jinsi ofisi yake inavyojipanga kuibua vipaji vya michezo mbalimbali kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari za kwenye Halmashauri hiyo.

Na Amon Mtega,Mbinga.

AFISA Elimu wa Sekondari katika Halmashauri ya Mbinga mji Stuart Kuziwa amesema ofisi yake inajipanga vema kuinua vipaji vya michezo kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari za kwenye Halmashauri hiyo na hatimaye kufanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali yakiwemo ya Umiseta.

Akizungumza na mtandao huu afisaelimu huyo amesema kuwa ofisi hiyo imefikia kufanya maandalizi ya wachezaji wa michezo mbalimbali kwa kuwaibua wanafunzi kwenye shule zao wanazosoma baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanavipaji vya michezo lakini havionekani kutokana na kutokuibuliwa.

Kuziwa amesema kuwa hadi sasa wanafunzi 100 wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu wameshapatikana na siku siyo nyingi watapelekwa kabini ili kuwanoa kikamili na mwisho wa siku kuwa na vijana bora wa michezo.

Amefafanua kuwa licha ya kuwa na vijana bora kwenye nyanja za michezo lakini bado katika mashindano ya Umiseta watafanya vizuri kwa kuwa watakuwa wameandaliwa vya kutosha.

Akizungumza kwa mifano afisa elimu huyo amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiidharau michezo bila kutambua faida zake kuwa ni sehemu ya upataji wa ajira pamoja na kutengeneza afya za wachezaji.

Mratibu wa mashindano maalumu wa michezo Yovin Mapunda akizungumzia jinsi walivyojipanga kimichezo kwa Wanafunzi hao.

Kwa upande wake mratibu wa mashindano na mtaalamu wa michezo Yovin Mapunda amesema kuwa zaidi ya shule za Sekondari 20 zimehusishwa kikamilifu katika kupata wanafunzi wenye vipaji vya michezo.

Mapunda ambaye pia ni mdhibiti ubora wa shule amesema kuwa katika kuwapata wachezaji hao walifanya mabonanza mbalimbali kisha kuwapata wenye vipaji na kuwa wataendelea kuziita timu mbalimbali ikiwemo ya Sekondari Luhuwiko ya Songea kuwachezesha michezo ya kirafiki ili kuwajengea ujasiri vijana wao ikiwemo na kuvizoea viwanja mbalimbali vya michezo.

Post a Comment

0 Comments