Mbunge wa Jimbo la Manyoni mashariki Dkt Pius Chaya akikabidhi mchango wake kwa waumini wa Kanisa la Anglikana . |
Na Amon Mtega,Manyoni.
MBUNGE wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mkoani Singida Dkt Pius Chaya ameichangia kwaya ya Kanisa kuu la Roho zote la Anglikana sh.500,000 (Laki tano) kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya uimbaji kwenye kanisa hilo.
Dkt Chaya ametoa mchango huo wakati aliposhiriki ibada ya pamoja na waumini wa kanisa hilo siku ya Jumapili huku akiupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kusimamia vema miradi mbalimbali ya kanisa hilo ikiwemo ujenzi wa majengo ya shule ya awali ambapo mbunge huyo amechangia tofali 500(Miatano) ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za ujenzi huo.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni mashariki Dkt Pius Chaya akiwa mbele ya kanisa la Anglikani wakati akitoa salamu mbalimbali zikiwemo za kibunge. |
Mbunge Dkt Chaya wakati akichangia michango hiyo pamoja na kutoa salamu mbalimbali zikiwemo za kibunge kwenye kanisa hilo ambalo ni Diocess of Rift Valley(DRV) Mjini Manyoni huku ibada hiyo ikiongozwa na Canon Daud Manase amesema kuwa amefurahishwa na kazi zinazofanywa na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu John Lupaa kwa kushirikiana na waumini wao hivyo ameona kuna kila sababu ya kuunga mkono maendeleo hayo kwa kuchangia.
Amesema kuwa licha ya maendeleo yanayofanywa na Kanisa hilo lakini bado limekuwa likishirikiana na Serikali katika kuiletea maendeleo jamii ,huku mbunge huyo akiahidi kuishauri Serikali kuendelea kuboresha mahusiano katika Chuo cha Nursing pamoja na Hospitali ya Kilimatinde kutokana na historia kubwa ya kwenye bonde la Ufa.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni mashariki Dkt Pius Chaya akiwa amesimama bungeni kuwasilisha hoja mbalimbali za Wananchi wa Jimbo la Manyoni mashariki. |
Aidha katika hatua nyingine Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo ya salamu kutoa mrejesho wa fedha ambazo Jimbo limepokea kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,ikiwa ni pamoja na fedha zaidi ya Sh.Bilion 3.5 za UVIKO 19,huku akiwataka waumini waendelee kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita ili izidi kuwaletea maendeleo.
Pia mbunge Dkt Chaya amesema kuwa ofisi ya mbunge ipo wazi muda wote kwaajili ya kusilikiliza na kutatua kero za wananchi hivyo itaendelea kushirikiana na wananchi wa Jimbo hilo katika kuliletea maendeleo Jimbo hilo .
Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wakiongozwa na Canon Daud Manase wamemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea kwenye jamii huku wakimuombea kwa Mungu ili aendelee kuwa na Afya njema .
0 Comments