Mbunge wa Jimbo la Ulanga mkoani Morogoro Salim Alaudin Hasham amekabidhi matrekta matatu yenye thamani ya shilingi Milioni 150 kwaajili ya kuwasaidia wananchi kipindi hiki cha kilimo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mwaya wakati wa kukabidhi matrekta hayo Amesema hiyo ni moja ya ahadi yake aliyoiahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wakati akiomba kura hivyo ameona afanye haraka kwani anajua uhitaji wa matrekta katika jimbo lake ni mkubwa.
Aidha Mbunge Salim amewatoa hofu wananchi juu ya Taratibu za upatikanaji wa matrekta hayo kwa kuwahakikishia kuwa hayatakuwa na upendeleo wowote bali kila mwenye uhitaji atakayetoa taarifa katika ofisi yake basi atapatiwa kwa utaratibu maalum.
Mbunge Salim Alaudin ameongeza kuwa bado matrekta mengine yanaendelea kuja hivyo ni vyema wananchi wakayatunza haya matatu ili yatakapo kuja mengine yaweze kuwasadia wananchi kwa haraka na kuwawezesha kulima kisasa zaidi.
Wananchi wa Wilaya ya Ulanga kwa asilimia 80 wanategemea kilimo kwaajili ya kujiendesha kimaisha hivyo upatikanaji wa trekta hizo utawawezesha kulima kwa tija na kuwaletea manufaa makubwa bila kuwa na changamoto kubwa.
0 Comments