Idara ya Ardhi mkoani Morogoro imetajwa Kuwa ndio idara inayongoza kwa kulalamikiwa na wananchi kujihusisha na vitendo vya Rushwa .
Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Manyama Tungaraza wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema kwa kipindi Cha mwezi Julai hadi septemba mwaka huu wamepokea jumla ya taarifa 66 kwenye idara 22 ambapo Kati ya hizo idara ya Ardhi wamepokea malalamiko 24 ikifuatiwa na TAMISEMI 19.
0 Comments