SAFARI NI FUPI SANA



Msichana alikuwa amekaa kwenye Bus, iliposimama akaingia Mama Akakaa karibu na Yeye, akawa anamfinya na kumsukuma na mikoba yake mikubwa, Bwana mmoja akaona yanayotendeka, kwa hasira akamuuliza Yule Msichana, Kwanini huzungumzi husemi kitu Yale anayokufanyia huyu Mama mwenye kelele?? Binti akajibu akitabasamu "Sio lazima niwe mkali na kuzungumzia kila kitu "Safari ni fupi sana" na nitateremka kwenye kituo stage inayofuata..

Haya maneno "Safari ni fupi sana" yanafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, na tuyatumie kwenye shughuli zetu za kila siku.

Tunapojuwa Kuwa safari yetu hapa duniani ni fupi basi Hakuna Haja ya kudhulumu, wala mijadala isiyokuwa na faida, kukosa kuwasamehe wengine, kuwa na tabia mbaya, kukosa kushukuru wema..

Je, kuna mtu ameuvunja Moyo wako? Kuwa Mtulivu *"Safari ni fupi"*

Je, kuna mtu alikudharau, akakudanganya, Kuwa Mtulivu *"Safari ni fupi"*

Dhuluma yoyote ambayo umefanyiwa Kumbuka *"safari ni fupi"*

Wamesahau wema wako na kusimama na wewe, kuwa Mtulivu *"Safari ni fupi"*

Hawakukupatia haki yako, hawakukuheshimu, Kuwa Mtulivu *"Safari ni Fupi* " 

Tujaze Nyoyo zetu Mapenzi na amani na kushukuru Neema za Mwenyezi Mungu juu yetu,  safari yetu hapa ni fupi,  na hatutaregea tena tukiondoka,  

Hakuna anaejua muda Wa kuondoka kwake,  tuwe watulivu,  wazuri,  wenye kuzuia hasira, wenye kusubiri,  kusameheane na wengine,  tujishughulishe wakati wetu kwa yatakayo tusaidia Duniani na Ahera na yanayomridhisha Mwenyezi MUNGU mwingi wa rehema.. 

Tukumbuke *_"Safari ni Fupi".._*

Post a Comment

0 Comments