JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM WILAYA YA MBINGA YAPONGEZWA KWA UBUNIFU.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho akizungumzia ubunifu unaofanywa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbinga.

Na Amon Mtega,Mbinga.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Ruvuma Oddo Mwisho amewapongeza Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani humo kwa kuiamsha Jumuiya katika utendaji kazi.

Mwisho amezitoa pongezi hizo kwenye kikao cha baraza kuu la Wazazi wa CCM Wilaya humo ambalo limehudhuliwa na wageni mbalimbali waalikwa akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda kwa lengo la kuwashirikisha kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo.
 
 
Mwenyekiti huyo amesema kuwa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mbinga ambayo mwenyekiti wake Ernest Mjilima pamoja na katibu wake Angelo Madundo imekuwa mfano kwa Jumuiya zingine za Mkoani humo kutokana na ufanyaji kazi wake ambao unapaswa kuigwa na Jumuiya hizo.

Amezitaja baadhi ya kazi ambazo zimefanywa na Jumuiya hiyo kuwa ni kuunganisha vikundi vya wajasiliamali ili vipatiwe mikopo, kufanya bonaza ambalo lililoendana na kufanya usafi katika maeneo ya Stendi,Soko na Hospitalini , kuimarisha miundombinu ya Sekondari ya Mkinga inayomilikiwa na Wazazi hao jambo ambalo jamii imetambua kuwa Jumuiya ya Wazazi inafanya kazi.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya Jumuiya kushindwa kubuni mambo mbalimbali ya maendeleo kwa jamii jambo limekuwa likirudisha nyuma jitihada za maendeleo ndani ya chama na jamii kwa ujumla.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbinga Ernest Mjirima (Mgogo) akizungumzia jinsi Jumuiya hiyo ilivyojipanga kufanya kazi.

Kwa upande wa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Ernest Mjirima (Mgogo) awali wakati akimkaribisha mwenyekiti  huyo wa mkoa amesema kuwa Jumuiya hiyo imejipanga kuhakikisha inaendelea kuchapa kazi kwa manufaa ya jamii na chama pia.


Hata hivyo mwenyekiti Mjirima amemshukuru mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye shule ya Sekondari ya Mkinga kuhakikisha inapatiwa umeme jambo ambalo litaifanya shule hiyo kuwa na ongezeko la ufaulu.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbinga Angelo Madundo akizungumzia maazimio mbalimbali yaliyofika na baraza hilo ikiwemo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali kwa manufaa ya jamii.

Naye katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbinga Angelo Madundo amesema kuwa baraza hilo limepitisha maazimio mbalimbali ikiwemo na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa madarasa yatokanayo na Uviko 19.

Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda akizungumzia jinsi wabunge wanaotokea majimbo ya Mbinga watakavyoendelea kushirikiana na Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi CCM katika suala zima la maendeleo.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda wakati akitoa salaam kwenye baraza hilo amesema kuwa wabunge wanaotoka kwenye majimbo ya Mbinga wataendelea kushirikiana na chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na Jumuiya zake zote katika kuwaletea maendeleo kwenye jamii.

Afisa maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mbinga Vijijini Pascal Ndunguru akitoa Elimu ya ujasiliamali kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM ili kuendana sambamba na kauli ya Siasa na Uchumi.

Aidha wajumbe wa mkutano huo kabla ya kujadili taarifa walipatiwa mafunzo ya ujasiliamali yaliyotolewa na Afisa maendeleo ya jamani wa Halmashauri ya Mbinga Vijijini Pascal Ndunguru ambaye amewataka Wazazi hao kwenda kutimiza kaulimbiu ya Siasa na Uchumi ili kuimarisha Jumuiya hiyo na Chama kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments