Kila mmoja huishi akitamani afanikishe jambo Fulani katika maisha yakeblakin kuna vikwazo huweza kupelekea kushindwa timiza.
Wakati wengine wakiumaliza Mwaka kwa furaha huenda kwa sababu
Wamefaulu shule
Wamepata mkopo wa chuo
Wamepata ajira
Wame OA au KUOLEWA
Wamepata mtoto
Lakini kuna mwingine anaumia kwa kukosa hayo hayo mambo
Kafaulu lakin kakosa mkopo,hivyo yupo mbioni kuacha chuo.
Kaoa au kuolewa ila mpaka sasa hakuna mtoto.
Mwingine aliahidiwa kuoa au kuolewa Mwaka huu lakin kaambulia Usaliti au magonjwa juu... Aliye mtegemea kaingia mitini au kabebwa na wengine.
Mwingine kajikuta akiumaliza Mwaka kwa ndoa yake au mpenz wa mda mrefu kuachana nae.
Lakini yupo ambae kaishia kuzika watu muhimu kwake
Yote kwa yote
Haijalishi umefeli katika lipi
Shukuru Mungu bado upo hai
Hivyo unayo nafasi kujaribu tena kesho... Huwezi kujilinganisha na mtu aliyefariki maana Hana tena nafasi ya kutimiza mambo yake.
Mioyo yetu ina wingi wa huzuni lakini tunapaswa tutambue kuwa kila jambo hupangwa na Mungu.
Muda utafika nasi tutafanikisha tunayo yaombea kila siku.
Hongera kwa wanao umaliza Mwaka kwa kufanikisha sehem ya ndoto zao hasa ktk kupata ndoa au familia..wengine tusubiri wakat watu.
Usiharakishie Ndoa halafu kesho ukajuta. Umri usikufanye utamani KUOA au KUOLEWA,bora uchelewe lakini umpate mtu sahihi.
0 Comments