SERIKALI YAWAPONGEZA WAWEKEZAJI WAZAWA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Pr,Carolyne Nombo akikata utepe kuashilia kufungua kwa majengo ya Chuo cha Ufundi stadi cha Top one in (V.T.C)kilichopo kata ya Mshangano Manispaa ya Songea kushoto ni mkurugenzi wa Chuo hicho Pascal Msigwa.

Na Amon Mtega,Songea.

NAIBU katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amewapongeza wawekezaji wazawa wanaowekeza katika sekta ya Elimu kwa kuwa wanasaidia Serikali kuelimisha jamii.



Pongezi hizo amezitoa wakati akizindua majengo ya Chuo cha Ufundi stadi cha Top one in (V.T.C) yaliyopo eneo la Msiendembali kata ya Mshangano katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ambayo imeenda sambamba na mahafari ya 12 ya chuo hicho huku wahitimu wakiwa 39.



Akizungumza kwenye uzinduzi huo ambao ulitanguliwa na ibada maalum ya kukiombea chuo hicho kwa Mungu ili majengo hayo yatumike ipasavyo katika utoaji wa Elimu ya ufundi, Profesa Nombo amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wawekezaji wazawa kutokutambua umuhimu wa kuwekeza kwenye Elimu jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma jitihada za maendeleo ya Serikali katika nyanja ya Elimu.



"Naomba niwapongeze sana wawekezaji wazawa akiwemo mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi stadi Top one in (V.T.C) Pascal Msigwa kwa kuweza kwenye suala la Elimu jambo ambalo litaisadia kupanua uwigo wa Elimu  kwenye jamii yetu ambayo nyingi ili ilikuwa inakosa fursa ya Elimu hiyo"amesema Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo.

 

Aidha Naibu katibu Mkuu huyo akipokea risala iliyosomwa na  mwanachuo Mariam Alex ambaye ni muhimu wa Chuo hicho amesema kuwa changamoto zilizo ainishwa kwenye risala hizo Wizara yake itaenda kuzifanyia kazi ikiwemo na kulingana na ubora wa miundombinu iliyopo chuoni hapo kuona namna ya kukipatia hadhi kiweze kutoa hadi mafunzo ya ngazi ya Diploma


Mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za mikoa ya juu ,Suzan Mgani akiahidi kuendelea kushirikiana na chuo Cha ufundi stadi cha Top one in (V.T.C)katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazojitokeza kwenye chuo hicho.

Kwa upande wake mkurugenzi wa VETA wa mikoa ya kanda ya nyanda za juu ,Iringa,Njombe Suzan Mgani amesema kuwa Veta imekuwa ikishirikiana na Chuo Cha ufundi stadi Top one in tangu kilipoanzishwa takribani miaka 12 sasa na kuwa kimeendelea vizuri kiasi Cha kuwa na majengo mazuri ya kisasa yenye hadhi ya chuo.



Mkurugenzi Mgani amesema kuwa hadi sasa wataendelea kushirikiana kikamilifu ili kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaweza kurudisha nyuma jitihada za chuo hicho ambacho tayari kimekuwa tegemeo kwa jamii mbalimbali hapa Nchini.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea Mjini ,Hamis Abdalah Ally akiwataka wakazi wa Songea kukitumia chuo hicho kama sehemu ya fursa kwao.

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Mjini Hamis Abdalah Ally amempongeza mkurugenzi wa chuo hicho Pascal Msigwa kwa kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi stadi hapa Nchini na Manispaa ya Songea huku akiwataka wakazi wa Songea kutumia fursa hiyo.


Mkurugenzi wa Chuo Cha Top one in (V.T.C) Pascal Msigwa akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wawekezaji wazawa .

Pia mkurugenzi wa Chuo hicho Pascal Msigwa ameishukuru Serikali inayoongonzwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali wawekezaji wazawa na kuwa awali wakati wa ujenzi wa majengo hayo alipata misukosuko sana ya kuhamishwa maeneo ya kujenga ikiwemo kuvunjiwa majengo yaliyokuwa yakijengwa kwenye maeneo hayo.


Paroko wa parokia ya Tanga Jimbo la Songea kanisa la Romani Katholiki ,Susey Joseph akibariki majengo ya Chuo Cha ufundi stadi Cha  Top one in (V.T.C)ili Mungu akibariki  chuo hicho.

Awali Paroko wa kanisa la Romani Katholiki katika parokia ya Tanga katika Jimbo la Songea Susey Joseph akihubiri kwenye uzinduzi huo huku akiyamwagia maji ya baraka kwenye majengo ya Chuo hicho amesema kuwa Elimu itakayotolewa hapo ni kwa manufaa ya jamii nzima hivyo Mungu anatambua kazi iliyofanywa na familia ya Pascal Msigwa kuwa ni la kitume.









Post a Comment

0 Comments